KISIMA CHA MAJI KIPUNGUNI, HUDUMA IMEREJEA
26 Feb, 2025

Kazi ya matengenezo ya miundombinu ya mabomba ili kuboresha upatikanaji wa huduma katika Kisima cha Maji Kipunguni "B kilichopo kata ua Ukonga imekamilishwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) na huduma kuanza kurejea kwa Wananchi.
Matengenezo hayo yamefuatila hitilafu iliyojitokeza na kusababisha kusimama kwa uzalishaji maji katika Kisima hicho kinachohudumia Wakazi takribani 1,000.
Kazi ya matengenezo imekamilika na zoezi la ujazaji wa Tenki linaendelea ili kurejesha huduma katika hali ya kawaida kwa wakazi hao wanaohudumiwa na Mkoa wa Kihuduma wa DAWASA Ukonga.