KWEMBE KWA BIBI CHOROBI HALI SHWARI, HUDUMA YAIMARISHWA
03 Oct, 2025
Kazi ya kuboresha bomba la maji lenye ukubwa wa inchi 8 lililopata hitilafu na kupasuka ikitekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) katika eneo la Kwembe kwa Bibi Chorobi.
Kazi hii inalenga kuimarisha huduma kwa wateja wanaohudumiwa na Mamlaka katika maeneo ya Mloganzila Kibamba Hospital, Mnazi Mmoja pamojna na Mji mpya.
Mamlaka inaendelea na jitihada za kuboresha huduma ya maji katika eneo lake lote la kihuduma katika mikoa ya Dar Es Salaam na Pwani ili kuhakikisha dhamira ya Serikali kumpatia kila mwananchi huduma ya majisafi inatimia.
