Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
MAADHIMISHO SIKU YA WAHANDISI YAFIKA TAMATI, DAWASA YAPONGEZWA
30 Sep, 2025
MAADHIMISHO SIKU YA WAHANDISI YAFIKA TAMATI, DAWASA YAPONGEZWA

Mkutano maalum wa siku ya Wahandisi Kitaifa ulioratibiwa na Bodi ya Wahandisi Tanzania (ERB) umemalizika huku Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) ikipongezwa kwa ushiriki wenye tija.

Mkutano huo ulianza Septemba 25 hadi 26, 2025 katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam na kushirikisha Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi kufanya maonesho ya huduma na bidhaa wanazozitoa. 

Wananchi mbalimbali waliofika katika banda la DAWASA wameipongeza Mamlaka kwa kushiriki maonesho haya kwani imekuwa fursa ya kuwasogezea huduma karibu na kufahamu mipango mbalimbali ya Mamlaka katika kufikisha huduma za Maji.

"Imekua fursa kubwa sana kwa DAWASA kushiriki nasi hapa, tumeweza kupata elimu juu ya huduma za maji, tumejionea kuanza kwa matumizi ya Mita za malipo ya kabla yaani Pre-paid meters, utekelezaji wa miradi ya kimkakati kama vile Kidunda lakini zaidi wengi tumesikilizwa changamoto zetu na kutatuliwa," amesema Hafidh Ally.