MABORESHO CHEMBA ZA MAJITAKA SINZA A
26 Oct, 2024

Kazi ya uboreshaji wa chemba za majitaka pamoja na uwekaji wa mifuniko ya chemba hizo mtaa kwa mtaa ikiendelea katika mtaa wa Sinza A, Wilaya ya Kinondoni chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA).
Kukamilika kwa maboresho haya kutaongeza ufanisi katika mifumo ya majitaka, na kuboresha usafi wa mazingira kwa kuzuia taka ngumu kuingia katika mifumo chemba hizo na kusababisha uzibaji wa mara kwa mara unaopelekea uchafuzi wa mazingira kwa majitaka kutiririka mitaani.
USAFI WA MAZINGIRA NI UTU.