Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MABORESHO HUDUMA YA MAJI GOBA
20 Aug, 2024
MABORESHO HUDUMA YA MAJI GOBA

Kazi ya kuweka toleo la bomba la inchi 3 kutoka bomba la usambazaji maji la inchi 4 inaendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika eneo la Simba Oil

Kazi hiyo inahusisha utolewaji wa maji katika bomba la inchi 4 kuelekea bomba la usambazaji maji la inchi 6 pamoja na ulazaji wa bomba la inchi 3 umbali wa mita 60 ili kuongeza msukumo maji katika eneo ilo. 

Kukamilika kwa kazi hiyo itasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Simba Oil, Chasimba, Minji, River View, Goba Zahanati, Shimbi Kati na Mwamuyamu.