MABORESHO HUDUMA YA MAJI GOBA - MAGETI
25 Sep, 2024

Kazi ya kuchepusha maji kutoka tanki la Tegeta A kuingiza kwenye bomba la usambazaji maji la inch 4 inaendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika eneo la Tegeta A
Kazi hiyo inahusisha utolewaji wa maji katika bomba la inchi 6 kuelekea bomba la usambazaji maji la inchi 4 ambayo yataelekezwa kwenye bomba la inchi 1.5 ili kuongeza msukumo maji katika eneo la Mageti.
Kukamilika kwa kazi hiyo itasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Mageti Sheli, Savana, Bosheni, Vumilia na Luisi Shule.