MABORESHO HUDUMA YA MAJI KIGAMBONI - GOMVU
12 Nov, 2024

Kazi ya matengenezo ya bomba lililopo katika eneo la Shule ya Msingi Gomvu ikitekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa kihuduma Kigamboni.
Matengenezo hayo yanahusisha bomba la inch 1 kwa kubadilisha kipande cha mita 15 kililoharibika kutokana na shughuli mbalimbali za kijamii katika eneo hilo.
Kukamilika kwa kazi hii kumeimarisha upatikanaji wa huduma kwa wakazi takribani 980 wa maeneo ya Shule ya Msingi Gomvu, Kata ya Somangira mtaa wa Kichangani.