Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MABORESHO HUDUMA YA MAJI KIJITONYAMA
12 Feb, 2025
MABORESHO HUDUMA YA MAJI KIJITONYAMA

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Kinondoni wanaendelea na kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika bomba lenye ukubwa wa inchi 8" eneo la Alimaua wilaya ya Kinondoni.

Kazi hii inahusisha kudhibiti uvujaji katika bomba la inchi 8" na kufanya toleo katika bomba la inchi 4".

Kukamilika kwa kazi hiyo kutarejesha na kuboresha huduma ya maji katika maeneo ya Alimaua 'A', Alimaua 'B', Mpakani 'A', Bwawani, Mwenge na Nzasa.