MABORESHO HUDUMA YA MAJI KITOPENI
31 Aug, 2024

Kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika bomba la usambazaji maji lenye ukubwa wa inchi 6 katika eneo la Kitopeni karibu na kituo cha kusukuma maji Kitopeni imetekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Kazi hiyo imehusisha kubadili kipande cha bomba kilichoathiriwa ili kudhibiti upotevu wa maji uliopelekea baadhi ya maeneo kukosa huduma ya maji.
Kukamilika kwa kazi hiyo itasaidia kurejesha na kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya
Makabe kanisani, Juhudi, Mngazija, Maarifa, Upendo, Kwa mgondo, Kanani, Mtaa wa orange, Mtaa wa mahenge, Kavimbirwa, Tabata, Tarakea, Mtaa wa misri, Dady street, Mtaa wa Mwakaleli, Kwa Moyo na Aureke.