MABORESHO HUDUMA YA MAJI MABIBO - EXTERNAL
29 Nov, 2024
Kazi ya matengenezo ya bomba kubwa la inchi 6 katika eneo la Mabibo External Kata ya Mabibo Wilaya ya Ubungo ikitekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma Magomeni.
Matengenezo hayo yanahusisha kubadilisha bomba na kuweka lingine kwa umbali wa mita 720.
Maboresho haya yanalenga kuongeza ufanisi na kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wakazi takribani 600 wa maeneo ya Azimio, Kanuni, Jitegemee, Matokeo, Midizini na Kilimahewa.