MABORESHO HUDUMA YA MAJI MSAKUZI KAZI INAENDELEA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na kazi ya uboreshaji upatikanaji wa huduma ya maji safi katika maeneo yake ya kihuduma ikiwa ni lengo la kuwapatia wateja wake huduma bora wakati wote.
Maboresho hayo yanahusisha uchimbaji na ulazaji wa bomba za ukubwa wa inchi 2 na inchi 3 kwa umbali wa kilomita 5.3
Akizungumzia kazi hiyo, Meneja mkoa kazi wa kihuduma DAWASA Ubungo Mhandisi Damson Mponjoli amesema maboresho hayo yanaendelea kufanyika kwa kasi ambapo hadi sasa kazi inayoendelea ni kulaza bomba katika mitaa ambayo inachangamoto ya huduma.
Kukamilika kwa kazi hiyo, kutaimarisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Msakuzi kwa Mkapa, Kwa Makoko na Msakuzi zizi la Ng'ombe na kuhudumia takribani wakazi 500 wa maeneo hayo.
