Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MABORESHO HUDUMA YA MAJI SALASALA
18 Jul, 2024
MABORESHO HUDUMA YA MAJI SALASALA

Kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika bomba la usambazaji majisafi lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 12”  imetekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika eneo la Salasala.

Kukamilika kwa kazi hiyo kumesaidia kurejesha na kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wakazi zaidi ya 3000 wa maeneo ya Njia Panda ya Kinzudi, Mtaa wa Oraah, Tatedo, Kwa Ulomi, Kwa Ndamba, Mwaikombo, Mwakalapa, Saleko na Kurungu.

Ni kipaumbele cha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam kuhakikisha huduma zinatolewa kikamilifu kwa viwango bora.