MABORESHO YA HUDUMA BUNJU KILUNGULE HADI MOGA
27 Jun, 2024

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inaendelea na kazi ya kuweka toleo la bomba lenye ukubwa wa inchi 12 kutoka bomba la inchi 54 eneo la Bunju Mianzini.
Kazi itasaidia kuboresha huduma ya maji katika maeneo ya Bunju A, Bunju B, Bunju Kilungule kwa Makala, Bunju Beach, Bunju Mkoani, Kihonzile, Kotela, Burumawe, Mbweni, Boko Basihaya, Ununio,Tegeta, Bahati beach na Moga.
Kazi inafanyika usiku na mchana kuhakikisha huduma inarejea kwa Wananchi.
Endelea kuwasiliana na kituo cha huduma kwa Wateja 0800110064 (Bure)
Imetolewa
Kitengo cha Mawasiliano