MABORESHO YA HUDUMA HANANASIFU
15 Jun, 2024

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Kinondoni wakiendelea na kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika bomba la inchi 3 eneo la Mashineni Kata ya Hananasifu Wilaya ya Kinondoni.
Kukamilika kwa kazi hiyo kutaimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi zaidi ya 350 katika maeneo ya mashineni, juhudi sekondari, kawawa, mkunguni A na B.