MABORESHO YA HUDUMA KISARAWE
06 Jun, 2024

Mafundi wa DAWASA Mkoa wa kihuduma Kisarawe wakiendelea na kazi ya kudhibiti uvujaji wa maji katika bomba la kipenyo cha inchi 3 Mtaa wa Pugu Kona na la inchi 2 katika Mtaa wa Bane, Wilaya ya Ilala.
Kazi hiyo inasaidia kupunguza upotevu wa maji na kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wakazi zaidi ya 1,200 waliopo katika maeneo ya Pugu Kona, Bane kwa Maswi na Dunda A Forest.
Mamlaka inawahimiza wateja na wananchi wanapoona uvujaji kutoa taarifa kwa haraka kupitia namba 0800110064 (bure) au 0735202121 (Whatsapp tu).