MABORESHO YA HUDUMA YA MAJI CHANGANYIKENI
18 May, 2025

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma Makongo wanaendelea kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika eneo la Changanyikeni
Kazi hii inahusisha kubadilisha kipande cha bomba kilichoathirika katika bomba la usambazaji maji lenye ukubwa wa inchi 8
Kukamilika kwa kazi hii kutaboresha na kurejesha Huduma ya maji kwa wakazi wa Mtipesa, Barabara ya Shule, Goba Center, Cantina na Kibululu