MABORESHO YA HUDUMA YA MAJI MAKONGO CCM
16 Jan, 2025

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wanaendelea na kazi ya kudhibiti uvujaji wa maji katika bomba lenye ukubwa wa inchi 6 eneo la Makongo CCM Karibu na ofisi za Serikali ya Mtaa
Kazi hii inahusisha kufunga kipande cha bomba katika eneo la bomba lililoathirika ili kutibu uvujaji huo.
Kukamilika kwa kazi hiyo kutarejesha na kuboresha huduma katika maeneo ya Kwa Sanya, Madukani, Kwa Mzee Juma, Boda Point, Gold Star CCM, Mji Mpya, Kagoma Road, Kwa Baba Jesca, Kwa Yebo na Ukololo