MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA HUDUMA YA MAJI KIMARA MAVURUNZA
10 Jun, 2024

Kazi ya kuongeza msukumo wa maji katika bomba la usambazaji maji eneo la Kimara Mavurunza inatekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Kazi hiyo imehusisha ulazaji wa bomba zenye ukubwa wa inchi 8 kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji.
Kukamilika kwa kazi kutaboresha huduma kwa wakazi wa maeneo ya;
Makongo Juu, Kanisa Katoriki, Kwa Majata, Kona ya Ajabu na Sakuveda.