MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MAJI CHALINZE
01 Oct, 2024

Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia mkoa wa kihuduma DAWASA Chalinze imefanya maboresho ya miundombinu ya maji katika bomba la inchi 9 eneo la Lulenge linalopeleka maji kwa wananchi wa Vijiji vya Tukamisasa, Ubena Zomozi, Lulenge mpaka bwawani.
Maboresho hayo yamefanyika ili wananchi wa maeneo tajwa kunufaika na huduma ya maji waliyoikosa kwa zaidi ya miaka 15 tangia kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa maji chalinze awamu ya pili.