Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MAJITAKA MWENGE - ITV
15 Jun, 2024
MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MAJITAKA MWENGE - ITV

Kazi ya kutoboa barabara kulaza bomba ya majitaka yenye ukubwa wa inchi 16 ikiendelea katika eneo la Mwenge - ITV ikiwa ni hatua za mwisho za ukamilishaji wa kazi ya uboreshaji wa miundombinu ya majitaka eneo hilo iliyohusisha kubadilisha bomba chakavu la zege kwa umbali wa mita 90.

Kukamilika kwa kazi hii kutaboresha huduma kwa wakazi takribani 1,000 wa maeneo ya Mlimani city, Mwenge kwa masista, Mwenge round about, Mwenge TRA, Zahanati ya Mwenge pamoja na baadhi ya maeneo ya Sinza.