Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MATENGENEZO BOMBA KUBWA VISIGA, KAZI IMEKAMILIKA
24 Feb, 2025
MATENGENEZO BOMBA KUBWA VISIGA, KAZI IMEKAMILIKA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekamilisha kazi ya matengenezo ya dharura katika mabomba makubwa ya usambazaji maji yenye ukubwa wa inchi 24 na 30 eneo la Visiga yaliyolenga kuzuia upotevu wa maji na kuimarisha huduma kwa wateja wanaohudumiwa na Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu.

Kazi hii ilisababisha kupungua kwa uzalishaji maji kwa wananchi wa maeneo ya: Chalinze Mboga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa,Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Segere, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe.

Huduma ya maji inaendelea kuimarika katika maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na matengenezo hayo.

Kwa Mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au 0735 202 121 (WhatsApp Tu)

Imetolewa na 
Kitengo cha Mawasiliano