MATENGENEZO BOMBA KUBWA VISIGA, KAZI INAENDELEA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inaendelea na kazi ya matengenezo ya dharura katika mabomba makubwa ya usambazaji maji yenye ukubwa wa inchi 24 na 30 eneo la Visiga inayolenga kuzuia upotevu wa maji na kuimarisha huduma kwa wateja wanaohudumiwa na Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu.
Kazi hii imesababisha kupungua kwa uzalishaji maji kwa wananchi wa maeneo ya: Chalinze Mboga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa,Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Segere, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe
Kazi inategemea kukamilika mapema na kurejesha huduma katika hali yake ya awali.