MATENGENEZO RUVU JUU, KAZI INAENDELEA
11 Dec, 2024
Kazi ya matengenezo ya dharura katika Mtambo wa Uzalishaji maji wa Ruvu Juu inaendelea kutekelezwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kudhibiti uvujaji wa Maji katika maungio ya bomba kubwa la inchi 40 katika eneo la Mlandizi Mkoani Pwani.
Matengenezo hayo yalilazimu kuzimwa kwa Mtambo huo kwa Saa 24 kuanzia Desemba 10,2024 na kuathiri Wananchi wa maeneo kuanzia Mlandizi hadi Kisarawe.