Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MATENGENEZO YA BOMBA KUBWA ENEO LA PUGU
01 Oct, 2024
MATENGENEZO YA BOMBA KUBWA ENEO LA PUGU

Kazi ya matengenezo ya bomba la inchi 6 inaendelea kutekelezwa na mafundi waMkoa wa Kihuduma DAWASA Kisarawe katika eneo la Pugu Njia panda kwa Pinda.

Matengenezo yametokana na bomba hilo kupasuka chini ya ardhi kwenye lami na kusababisha uvujaji ambao umeathiri upatikanaji wa maji kwa wateja wa maeneo ya Pugu hadi Buyuni.

Kazi hii ya matengenezo imeanza Oktoba 1, 2024 na inatarajia kukamilika Oktoba 2,2024 ambapo itasaidia  kuboresha huduma ya maji kwa zaidi ya wateja 6,000 waliopo katika maeneo ya Pugu Bombani, Kigogo Fresh A na B, Relini Magnus, Mustafa, Kinyamwezi, Mgeule, Mgeule juu, Taliani, Nyeburu, Pugu Kajiungeni, Mwakanga, Buyuni, Kwa Mbiki, Kwa Zoo, Zavala, Dampo, na Chikila.