MBWEWE KUPATA UHAKIKA WA HUDUMA
22 Jul, 2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekamilisha kazi ya maboresho ya bomba la maji la inchi 6 katika eneo la Mbwewe, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, Meneja wa DAWASA Mkoa wa kihuduma Chalinze Mhandisi Boniface Philemon amesema maboresho hayo yamefanikiwa kuongeza ufanisi wa usambazaji wa maji na kupunguza changamoto zilizokuwa zikiathiri huduma kwa wakazi wa Mbwewe na maeneo jirani.
Amebainisha kuwa DAWASA itaendelea kutekeleza maboresho ya miundombinu ya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na endelevu.
