MHANDISI BWIRE AKUMBUSHA UWAJIBIKAJI ILI KUBORESHA HUDUMA KWA WANANCHI
10 Sep, 2025

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire awewakumbusha Watumishi kuwajibika kwa changamoto za kihuduma ili kuboresha huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira.
Mhandisi ameyasema hayo katika wakati wa zoezi la kusaini mikataba ya ufanisi, utendaji kazi na uwajibikaji unaolenga kuboresha utendaji kazi katika utoaji wa huduma.
Zoezi hilo limeshuhudiwa na Wakurugenzi, Meneja pamoja na viongozi waandamizi wa DAWASA