MHANDISI BWIRE ASHIRIKI MKUTANO SEKTA YA MAJI

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire ni miongoni mwa watumishi wa Sekta ya maji waliohudhuria mkutano wa wataalamu wa kada za Utawala na Rasilimali watu, Maendeleo ya jamii na Maafisa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma katika Sekta ya maji unaoendelea Jijini Dar es salaam.
Akitoa salamu Kwa Waziri wa maji Mh.Jumaa Aweso, Mhandisi Bwire ameeleza umuhimu wa mkutano huu kwa Sekta ya maji nchini na jinsi utakavyosaidia Sekta kwa ujumla.
"Kikao hiki ni muhimu kwa kukutanisha kada hizi za kimkakati katika Sekta yetu ya maji ili kuweza kuweka malengo na kuhakikisha maono na dhamira za Wizara na Taasisi zake yanatimia" ameeleza Mhandisi Bwire.
Bwire ameongeza kwa kumshukuru Waziri wa Maji Mh.Jumaa Aweso kwa kuzikimbilia taasisi za Maji nchini bila kuchoka kila wakati wanapohitaji muongozo wake kitendo ambacho kimefanya waweze kutekeleza majukumu ya Taasisi hizo kwa ufanisi.
Mkutano huu uliofunguliwa rasmi na waziri wa maji Mh.Jumaa Aweso utafanyika Kwa muda wa siku tatu kwanzia tarehe 14 - 16/11/2024 na umebeba kauli mbiu isemayo Rasilimali watu ni chachu ya maendeleo endelevu katika Sekta ya maji.