Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
MHANDISI BWIRE ASIMAMIA RATIBA MGAO WA MAJI, AKAGUA HUDUMA KINONDONI
15 Dec, 2025
MHANDISI BWIRE ASIMAMIA RATIBA MGAO WA MAJI, AKAGUA HUDUMA KINONDONI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire amekagua hali ya upatikanaji huduma ya maji katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kinondoni hususani Kata ya Mwananyamala na kushuhudia wananchi wakiendele kupata huduma ya maji kama ratiba ya mgao  inavyoelekeza.

"Jambo kubwa tunalosimamia ni kuhakikisha wananchi wanapata maji kulingana na ratiba inavyoelekeza, lakini zaidi kupita mitaani na kuhakikisha maji hayo yanawafikia wateja majumbani mwao" ameeleza Mhandisi Bwire 

Bwire ameongeza msisitizo juu ya swala la utunzaji wa maji pale yanapotoka wananchi wawe na utamaduni wa kutunza maji lakini pia kuyatumia kwa matumizi Sahihi.

Ndugu Miriam Ally Mkazi wa Mwananyamala ametoa shukrani zake kwa DAWASA Kwakutoa taarifa ya changamoto ya upungufu wa huduma ya maji lakini zaidi kuwapatia ratiba inayoonyesha ni lini kila eneo linapata huduma ya maji.

"Tunashukuru katika eneo letu tunapata huduma ya maji mara mbili kwa wiki siku ya Jumapili na Jumatano, ingawa tunafahamu changamoto  ya maji inayotukabili kwasasa, hii imesaidia kutupa utauari na ufahamu ni lini tujiandae kupata huduma ya maji, tunaomba ratiba hii izingatiwe ili pasitokee malalamiko" ameeleza Miriam 

Pamoja na Ukaguzi wa huduma ya maji Elimu juu ya utunzaji wa maji na ufahamu wa ratiba ya kupata maji ilitolewa kwa wananchi mbalimbali wa eneo la Mwananyamala.