Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MHANDISI BWIRE AWAPA MATUMAINI YA MAJISAFI WAKAZI WA TEMEKE
13 Nov, 2024
MHANDISI BWIRE AWAPA MATUMAINI YA MAJISAFI WAKAZI WA TEMEKE

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire ametembelea na kukagua upatikanaji wa maji katika mfumo wa usambazaji maji eneo la Viwanda (Barabara ya Pugu), Dar es Salaam na kutoa matumaini ya upatikanaji wa maji kwa wakazi na wafanyabiashara wa maeneo hayo kupitia maboresho yanayoendelea sehemu mbalimbali ya kuimarisha huduma ya majisafi. 

Katika zoezi hilo, Mhandisi Bwire ameambatana na baadhi ya Wakurugenzi na Wataalam wa Mamlaka kwa lengo la kukagua mfumo wa usambazaji maji kuanzia eneo la Veta hadi Kipawa  kwa lengo la kuboresha huduma ya majisafi katika eneo hilo linalohudumiwa na Mkoa wa kihuduma DAWASA Temeke.

Mhandisi Bwire amewaelekeza wataalam kuja na mapendekezo ya kitaalam yatakayokuwa suluhisho la kuboresha huduma ya Maji katika maeneo hayo.

"Lengo letu kama Mamlaka ni kuhakikisha wateja wetu wenye matumizi makubwa kama Viwanda na Taasisi pamoja na wateja wa majumbani wanapata huduma ya uhakika ya Maji, wataalam tumieni taaluma yenu ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma ya Maji ya uhakika," amesema. 

Katika Ziara hiyo, Mhandisi Bwire ameielekeza Idara ya Uzalishaji na Usambazaji maji kwa kushirikiana na Wataalam wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Temeke ili kupata suluhisho la muda mrefu pamoja na la muda mfupi katika kuboresha huduma ya Maji kwa wateja wanaohudumiwa na DAWASA Temeke.