MHANDISI KUNDO AKUTANA NA WADAU SEKTA YA MAJI NCHINI
25 Sep, 2024

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Kundo A. Mathew (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa Sekta ya Maji wanaoshughulika na Usambazaji wa madawa ya kutibu na kusafisha Maji Ofisi za Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) uliofanyika Jijini Dar es salaam.
Kikao hicho kimehudhuliwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire pamoja na Menejimenti ya DAWASA.