Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI YAIMARISHWA PUGU-BANE
12 Jun, 2025
MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI YAIMARISHWA PUGU-BANE

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA imeendelea na zoezi la uboreshaji wa miundombinu ya mabomba ya usambazaji maji kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma katika Mtaa wa Bane katika Kata ya Pugu Wilayani Ilala.

Msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Irene Kweka kutoka Mkoa wa Kihuduma wa DAWASA Kisarawe amesema kuwa maboresho hayo  yamekusudia kuimarisha upatikanaji na usambazaji wa huduma ya Maji na kupunguza uvujaji unaotokana na mabomba chakavu yaliyowekwa kipindi cha nyuma katika Mradi wa Jumuiya ya Watumia Maji katika Mtaa huo.

"Maboresho haya yanahusisha ubadilishaji wa mabomba ya inchi 1 na inchi 1.5 kwa umbali wa mita 300 ambayo yatasaidia kuboresha na kudhibiti upotevu wa maji na kuongeza msukumo wa maji hivyo kuwafikia wateja wote." Amesema Mhandisi Irene.

Kazi ya maboresho itanufaisha zaidi ya wateja 100 katika Mtaa huo ambao awali walikuwa na changamoto ya kupata maji kidogo kutokana na kupungua kwa msukumo wa maji.