Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MRADI WA BANGULO MWANAPINDI WASHIKA KASI
01 Sep, 2025
MRADI WA BANGULO MWANAPINDI WASHIKA KASI

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kuongeza mtandao wa huduma ya majisafi katika eneo la Mtaa wa Bangulo Mwanapindi, Kata ya Pugu Stesheni, Wilaya ya Ilala.

Mradi huu wa kusogeza mtando wa huduma ya maji kwa wakazi wa eneo la Mwanapindi ni matokeo ya mradi mkubwa wa Usambazaji maji Dar es Salaam ya Kusini (Bangulo)  uliotekelezwa na DAWASA kwa gharama ya Shilingi Bilioni 36.9 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

Mradi huo unalenga kusogeza upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa eneo la Mwanapindi, unahusisha kazi ya uchimbaji mitaro na ulazaji wa mabomba ya kipenyo cha inchi 1.5", inchi 2 na inchi 3 kwa umbali wa kilomita 12.75 ambapo hadi sasa  utekelezaji wa kazi hiyo umefikia asilimia 22.

Mhandisi Adam Makindai wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Ukonga amesema mradi huo upo katika hatua nzuri na unatekelezwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Septemba hadi Oktoba 2025.

"Kwasasa tumeshachimba mitaro na kulaza mabomba kwa umbali wa kilomita 2.85, tunaendelea katika eneo la Shina namba 4 na 5 ambapo hadi sasa utekelezaji umefikia asilimia 22, tunatarajia baada ya kukamilika kwa mradi huu, wakazi zaidi ya 500 wa Bangulo Mwanapindi watafaidika kwa kupata huduma ya majisafi na salama," amesema Mhandisi Makindai.