MTAA KWA MTAA KUHUMIZA ULIPAJI WA BILI ZA MAJI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la ufuatiliaji wa malipo ya bili za huduma ya maji kwa wateja wenye madeni ya muda mrefu na muda mfupi katika maeneo ya mikoa ya Kihuduma ya Ukonga na Kisarawe.
Zoezi hili linaendelea kutekelezwa katika maeneo ya kata za Gongolamboto, Pugu, Majohe, Pugu Stesheni, Chanika, Buyuni na Kisarawe linaenda sambamba na utoaji wa elimu kwa wateja kuhusu matumizi sahihi ya maji, ulinzi wa miundombinu ya maji na umuhimu wa kulipa bili za maji kwa wakati pamoja na kusitisha huduma kwa wateja wenye malimbikizo ya madeni ya bili za maji.
DAWASA inaendelea kuwasisitiza wananchi kulipia bili mapema ili kuepukana na usumbufu wa kusitishiwa huduma kutokana na kutolipa kwa wakati.