MTENDAJI MKUU DAWASA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire ameanza ziara katika mikoa ya kihuduma DAWASA kwa lengo la kuongea na Watumishi ambapo amesisitiza uwajibikaji wenye tija ili kuongeza ufanisi na kuchochea huduma bora za Majisafi na Usafi wa Mazingira.
Mhandisi Bwire ametembelea mikoa ya kihuduma DAWASA Ubungo na Mabwepande ambapo ametoa mwelekeo mpya wa Mamlaka katika kusimamia upatikanaji wa huduma na uimarishaji wa huduma bora kwa Wananchi.
“Kauli mbiu yetu ya sasa inasema DAWASA Moja, Nguvu Moja, Kazi iendelee na tukutane site. Hii inamaanisha kuwa tutatumia muda mwingi kwenda kwa Wananchi, kusikiliza na kutatua changamoto zao kama Mamlaka tuliopewa dhamana ya kuwahudumia. Watumishi wenzangj tusimamie hii na mimi pamoja na Menejimenti yangu tutakuwa mfano katika haya tuliyokubaliana.” aliongeza Mhandisi Bwire
“Tukubaliane kuwa na 3T zetu kati yetu Menejimenti na Watumishi ambazo ni Tuwezeshane, Tupimane na Tuwajibishane hii itatusaidia katika kupimana na kuchukuliana hatua pale inapobidi kwa ustawi wa Mamlaka yetu” Aliongeza Mhandisi Bwire
Katika ziara yake hiyo, Mtendaji Mkuu Bwire aliongozana na baadhi ya viongozi na Menejimenti ya DAWASA na ziara yake itaendelea katika Mikoa na maeneo mbalimbali ya kihuduma ya Mamlaka.