NCAA YAONGEZA MAARIFA UTOAJI HUDUMA DAWASA
19 Jun, 2025

Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wamefanya ziara ya mafunzo katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kupata ujuzi na kujifunza zaidi juu ya usimamizi bora wa huduma kwa wateja.
Katika ziara hiyo, NCAA imetembelea Mtambo wa Uzalishaji Maji Ruvu Chini pamoja na Mradi wa Maji Kigamboni kupitia visima virefu na kujionea na kujionea namna DAWASA inavyotekeleza shughuli za uzalishaji na usambazaji Majisafi kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) hutumia vyanzo vya maji ya chini ya ardhi katika miradi ya kijamii ya uchimbaji wa visima na kusambaza maji hayo kwa matumizi ya binadamu, wanyama wa kufuga na wa porini.