Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
RUVU JUU HAKUNA KULALA, KAZI INAENDELEA.
23 Sep, 2025
RUVU JUU HAKUNA KULALA, KAZI INAENDELEA.

“Hatutalala hadi kazi ikamilike” ni maneno ya Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji Maji DAWASA, Mhandisi Leonard Msenyele wakati kazi ya matengenezo ya dharura katika pampu za kusukuma maji mtambo wa Ruvu Juu jioni ya leo, Septemba 22,2025. 

Kazi hii inachukua muda zaidi ya Saa 16 hadi kukamilika kwake na kumeathiri upatikanaji wa huduma ya maji  kwa wakazi wa maneno ya Chalinze-Mboga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mabwawa, Visiga, Maili 35, Maili Moja, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi Kimara, Tabata Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Saranga, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe.

Matengenezo yanatarajia kukamilika usiku wa leo.