Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
SEGEREA, UBUNGO, TEMEKE, UKONGA SASA MAJI MWA MWA MWA
18 Mar, 2025
SEGEREA, UBUNGO, TEMEKE, UKONGA SASA MAJI MWA MWA MWA

Mradi wa kihistoria Bangulo wakamilika na kuanza majaribio

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa usambazaji Maji Dar es Salaam ya Kusini uliopo kata ya Bangulo, Wilaya ya Ilala na kuelezea kuridhika na hatua ya ukamilishwaji wa mradi ambao uko katika hatua za majaribio.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo mapema Machi 18, 2025 Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kutekeleza mradi wa usambazaji maji Dar es Salaam ya kusini  maarufu kama Mradi wa Bangulo na kuagiza kuanza kufunguliwa kwa Dawati la huduma kwa wateja katika maeneo nufaika iliwananchi kujitokeza na kuunganishiwa huduma ya Majisafi katika makazi yao.

Pia ameielekeza Mamlaka kuwaunganishia wananchi wa kipato cha chini huduma ya Majisafi kwa mkopo kupitia utaratibu maalum wa Mamlaka na makubaliano kurejesha kidogo kidogo kupitia ankara zao.

"Nimeshuhudia mradi huu wa Bangulo umekamilika kwa wakati na sasa mnaendelea na majaribio,  rai yangu kwa wananchi na DAWASA ni ulinzi wa mradi huu ili udumu" alisema Mhe. Aweso

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri ameeleza kuwa awali huduma ilikuwepo lakin ilikuwa ikipatikana kwa watoa huduma binafsi lakini kupitia utekelezaji wa mradi huu utaongeza upatikani wa huduma ya maji na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa DAWASA pindi wanapobaini uvujaji wa maji ili kupunguza upotevu wa Maji yanayozalishwa.

"Mradi huu unapata maji kutokea chanzo cha Maji Ruvu juu eneo la Mlandizi, gharama madawa pamoja na umeme ni kubwa hivyo wananchi mtoe taarifa pale mnapo baini upotevu wa maji," alisema Mhandisi Mwajuma.

Akitoa taarifa za utekelezaji wa mradi huo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire amesema mradi umetekelezwa kwa kipindi cha miezi 12, na umehusisha ujenzi wa kituo cha kusukuma maji katika eneo la Kibamba, ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji la lita milioni 9 eneo la Bangulo, ulazaji wa mabomba ya kusafirisha maji kwa umbali wa kilomita 108. Mradi utanufaisha wananchi 450,000 wa Majimbo matano ya uchaguzi ikiwemo Ukonga, Segerea, Ubungo, Ilala na Temeke utakapokamilika. 

"Kwa sasa utekelezaji wa mradi umekamilika kwa asilimia 100 na upo katika hatua za majaribio kabla ya kuanza kutumika," amesema Mhandisi Bwire.

Kwa naiba ya wananchi nufaika wa mradi huo, Diwani wa kata ya Pugu Stesheni Mhe. Juma Shabani amemshukuru Mhe. Waziri wa Maji na DAWASA kwa kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo kwa wakati  iliyokuwa ni kiu ya muda mrefu kwa wananchi wa maeneo hayo.

"Wakati ulipokuja kusaini mradi huu Mhe. Waziri pale Pugu wengi tuliona kama  ni hadithi lakini sasa huduma tumeanza kupata tunashukuru sana" alisema Mhe. Shabani