SHULE YA MSINGI MLIMANI WAPEWA ELIMU KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa elimu katika klabu ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shule ya Msingi Mlimani iliyopo Wilaya ya Ubungo huku ikisisitiza juu ya umuhimu wa kushiriki wa juhudi za kupunguza upotevu wa maji katika jamii.
Shule hiyo ni miongoni mwa shule 11 za mazingira zinazosimamiwa na kuendeshwa na DAWASA.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Kitengo cha Kuzuia Upotevu wa Maji wa DAWASA, Peter Shirima amesema umuhimu wa jamii kutambua dhana nzima ya upotevu wa maji na kushiriki kwa vitendo kupunguza upotevu wa maji katika jamii.
"Maji ni muhimu katika jamii na Serikali inatumia gharama kubwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi, hivyo ni jukumu letu sote kushiriki katika kupunguza upotevu wa maji katika eneo linalomzunguka, kwa kutoa taarifa kwa Mamlaka kama kuna upotevu wa maji kwa kupasuka kwa mabomba, wizi wa mji, mita kuharibika," amesema Ndugu Peter.
Naye Mwalimu Lazaro Mwanzo, mlezi wa klabu ya mazingira shuleni hapo ameishukuru Mamlaka kwa jitihada za kutoa elimu ya umuhimu wa maji pamoja na suala la ushirikishwaji wa jamii katika kupunguza upotevu wa maji shuleni hapo.
"Elimu ya ushirikishwaji wa jamii katika kupunguza upotevu wa maji iliyotolewa na DAWASA leo, tumeipokea na tutasimamia kwa wanafunzi kuitekeleza kwa vitendo na naishauri jamii kushirikiana kwa pamoja kwa kutoa taarifa DAWASA kwa kupiga namba 181 wanapoona mivujo ya maji au viashilia vingine vya upotevu wa maji katika maeneo yetu," amesema Mwalimu Lazaro.
Kwa upande wake, Mwanafunzi Abigael Peter, ambaye ni mwanachama wa klabu ya maji na usafi wa Mazingira kutoka shuleni hapo, amekiri kunufaika na elimu hiyo na kushukuru DAWASA kufika shuleni hapo na kutoa elimu juu ya ushirikishwaji wa jamii kushiriki kupunguza upotevu wa maji.
"Tunashukuru DAWASA leo kufika hapa shuleni kwetu na kutupatia elimu ya upotevu wa maji na tunaidi kuifanyia kazi kwa vitendo kwa kushiriki kutoa taarifa kwa walimu na wazazi pale tunapoona viashilia vya upotevu wa maji shuleni na hata nyumbani kwa kupiga namba 181 DAWASA Bure.
Mamlaka inaendelea kusisitiza jamii kushiriki katika kupunguza upotevu wa maji kwa kutoa taarifa pale wanapoona upotevu wa maji kwa kutoa taarifa kupitia namba ya Huduma Huduma kwa Wateja 181(Bure)
