Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
TAASISI ZA SERIKALI ZIIGE MFANO WA DAWASA KUKUTANA NA VIONGOZI WA MITAA - DC MAPUNDA
24 Feb, 2025
TAASISI ZA SERIKALI ZIIGE MFANO WA DAWASA KUKUTANA NA VIONGOZI WA MITAA - DC MAPUNDA

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe Sixtus Mapunda amezitaka Taasisi za Serikali kuiga ushirikishwaji wa DAWASA katika kuwatumia Viongozi wa Mitaa katika kuwashirikisha na kutatua changamoto za huduma kwa pamoja.

Ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kwa kuchukua hatua ya kukutana na Wenyeviti wa mitaa kuwasikiliza, kutambua changamoto zao na kutengeneza mahusiano yatakayorahisisha utoaji wa huduma.

Mhe Mapunda ameyasema hayo kwenye Kikao Kazi cha DAWASA na Wenyeviti wa mitaa katika wilaya ya Temeke na kueleza kuwa DAWASA wamefanya kitendo cha kuigwa na Taasisi zingine za Serikali zinazowahumia Wananchi moja kwa moja.

“DAWASA hii ni jambo kubwa mmefanya ambacho kinatakiwa kuigwa na Taasisi zote za Serikali na kupewa nguvu za kuwa endelevu. Mlichokifanya nyinyi mmerahisisha kazi yenu, sasa kazi yenu itakuwa rahisi kuliko mnavyofikiria, Wenyeviti wapo tayari kufanya kazi ila hawakuwa na mtu wa kufanya naye kazi” alisisitiza Mhe Mapunda

Aidha Mhe Mapunda ameahidi kuchukua hatua ya kukutana na Taasisi nyingine za Serikali zinazohudumia Wananchi moja kwa moja nazo ziweze kukutana na Wenyeviti wa mitaa na kuweza kuwasikiliza na kutatua changamoto zao.