Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA
19 Oct, 2024
TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire ameshiriki katika zoezi maalum la kujiandikisha kwenye daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.

Mhandisi Bwire anawakumbusha na kuhimiza wananchi wote ambao bado hawajajiandikisha waweze kujitokeza na kutimiza wajibu wao wa kujiorodhesha katika daftari la mkaazi la mpiga kura na hatimaye kushiriki kupiga kura katika uchaguzi huo.

Zoezi la Uandikishaji Wapiga kura limezinduliwa rasmi Oktoba 11, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoani Dodoma na linaendelea kufanyika nchini kote.

#DAWASA_tupo_tayari_kujiandikisha