UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI CHANGANYIKENI
25 Sep, 2024

Kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika Bomba kuu la usafirishaji lenye ukubwa wa inchi 16 ikiendelea katika eneo la Changanyikeni Shule chini ya usimamizi wa mafundi wa DAWASA.
Kukamilika kwa kazi hii kutaongeza ufanisi katika tenki la maji Changanyikeni na kuboresha huduma kwa wananchi wa Mtu pesa, West river, Down hill, Camp Verde, Barabara ya shule, Lastanza, Hekima, Precious, Camp stone, Goba hill, Sunset close, Kachembele, Kantina, Shama, Magufuli, Mji mpya, Barrier, na Nagambo ya moto wanaohudumiwa na tenki hilo.