Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI MAGOMENI MZIMUNI.... KAZI INAENDELEA
22 Jul, 2026
UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI MAGOMENI MZIMUNI.... KAZI INAENDELEA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na kazi ya uboreshaji wa miundombinu ya mabomba ya maji ili kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wateja zaidi ya 400 waliopo eneo la Mtaa wa Mpanda, kata ya Mzimuni Wilaya ya Kinondoni.

Maboresho hayo yanahusisha kazi ya kubadilisha bomba chakavu za inchi 3" kwa umbali wa kilomita 2.

Kazi hii ya maboresho ya miundombinu ya maji inatekelezwa na DAWASA mkoa wa kihuduma Magomeni.

Kukamilika kwa maboresho hayo kutaongeza upatikanaji wa maji na kuimarisha huduma kwa wateja 400 kwa wakazi wa maeneo ya Takadiri, Mpanda, Ubungo, Mwinyimkuu na Mtaa wa Iweke.