Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI MAKABE
01 Jul, 2024
UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI MAKABE

Zoezi la kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Makabe Nyota njema, Makabe Dubai na Ubata Kata ya Mbezi linaendelea kutelekezwa na mafundi  wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA).

Zoezi hilo limehusisha utoaji wa toleo kwenye bomba la inchi 10 kwa umbali wa mita 1000 kwenda kujazia maji kwenye bomba la inchi 6 , inchi 4 na bomba la inchi 3 yanayohudumia maeneo hayo.

Kukamilika kwa zoezi hilo kutanufaisha wakazi zaidi ya 200 wa maeneo tajwa, Mamlaka inaendelea na jitihada za kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya majisafi na ya kutosheleza.