UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI MBAGALA
07 May, 2024

Kazi ya uboreshaji wa msukumo wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo ya Mwembeni, Big Brother na Darajani kata ya Mbagala Kuu ikiendelea kutekelezwa kwa kasi na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
Kazi hiyo imehusisha ulazaji wa bomba za inchi 2 kwa umbali wa mita 30 ambapo wakazi takribani 1800 wa maeneo tajwa watapata huduma ya maji kwa msukumo mkubwa.