UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI MLANDIZI
07 Mar, 2025

Matengenezo la bomba la inchi 6 yakitekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA - Mlandizi) katika Kata ya Janga mtaa wa Ngeta Mlandizi Mkoa wa Pwani kwa lengo la kudhibiti upotevu wa maji uliosababishwa na kupasuka kwa bomba hili.
Maboresho haya yatasaidia kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi zaidi ya 300 wa maeneo ya Ngeta, Kimara, Makotopora, Kikongo, Lupunga, Mkino, Videte, Mwanabwito, Kidai, Madimla na kisabi.