UBORESHAJI USAFI WA MAZINGIRA KURASINI
15 May, 2024

Kazi ya kubadilisha bomba la majitaka lenye wa urefu wa inchi 20 ikiendelea eneo la Chuo Cha Polisi Kurasini chini ya mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) ili kuruhusu miundombinu hiyo kufanya kazi kwa ufanisi.
Kukamilika kwa kazi hii kutanufaisha wakazi wa maeneo ya Uwanja wa taifa, Twalipo, Mgulani, Chuo Cha Polisi, na Serengeti kwa kuboresha usafi wa mazingira na kuondoa hatari za magonjwa ya mlipuko.