UBORESHAJI WA HUDUMA YA MAJI KIGOGO
24 Jun, 2024

Kazi ya kudhibiti upotevu wa maji ikitekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Magomeni katika bomba la inchi 4 eneo la Kigogo Mapera, Kata ya Kigogo Wilaya ya Ubungo.
Kukamilika kwa kazi hii kutasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi zaidi ya 700 wa maeneo ya Mkwajuni, Kona boys, Soko la kabichi, Randa bar, Magenge mengi, Kwa magereza, soko la ndizi na Mbuyuni.
Mamlaka inaendelea kuwakumbusha wananchi pindi wanapoona uvujaji wa maji kwenye maeneo yao kutoa taarifa kwa haraka kupitia namba 0800110064 (Bure) au 0735 202 121 (WhatsApp tu).