UBORESHAJI WA HUDUMA YA MAJI KURASINI
22 Jan, 2025

Maboresho katika bomba la inchi 16 inatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika eneo la Kurasini kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Keko, Chang'ombe na Kurasini.
Mamlaka kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA - Temeke inaendelea na zoezi la ufuatiliaji wa hali ya maji ili kuhakikisha kila Mwananchi anapata Majisafi na Salama katika maeneo yanayohudumiwa na kupitia vyanzo vya Maji katika Mitambo ya Mtoni, Ruvu Chini kwa lengo la kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa msukumo mzuri.