UDHIBITI UPOTEVU WA MAJI CHALINZE
03 Jun, 2024

Kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika bomba la inchi 8 kata ya Lugoba Halmashauri ya chalinze, imetekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam Mkoa wa kihuduma DAWASA Chalinze.
Kukamilika kwa kazi hii kutarejesha huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo ya Lugoba, Lunga, Mavi ya ng'ombe, Saleni, Makombe na Kinzagu.