UIMARISHAJI HUDUMA YA MAJISAFI KAVIMBILWA
20 Nov, 2024

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma Makongo wakiendelea kazi ya kufungua valvu za kutoa upepo katika mitaa ya Kalali na Kavimbilwa, ili kuruhusu Maji kusafiri kwa msukumo mzuri.
Zoezi hili linalenga kuongeza msukumo wa maji yanayotoka katika tenki la Maji la Kitopeni na kupita katika bomba za usambazaji maji za inchi 6 na inchi 3 ambazo zitatatua changamoto ya msukumo mdogo wa maji pamoja na ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo ya wananchi.
Wataalamu hawa wako saiti kuhakikisha huduma ya maji inaimarika na kuwafikia wateja wa maeneo ya Kalali, Mwakaleli, Dadis, Kirumba, Orange, Misri, Madina, Ardhi, Mzangi na Kavimbilwa.